Like our Page

Yaliyopo

 

Retreat at Pfarre Gartenstadt

Dear St. Bakhita Community members,

We are all invited to a retreat @ Galvanigasse 1-3, 1210 Wien.

On 16 & 17th March 2018.

Friday: 18:00 - 20:00

Saturday: 9:00 - 20:00hrs

Retreat Master: Fr Nicholas Chileshe from Zambia.Talks will be in English and translated into Germany.All are welcome

**********

For More Details: www-gartenstadt.at

 

Ee viumbe karibuni .  I

1 Ee Viumbe, karibuni! Mungu wenu kamsifuni!

Kiitikio:  Ndiyo Sak:ramenti kuu, Mwili Damu ya Yesu.

2 Ee Maria, utaanza Kumwimbia we wa kwanza.

3 Nanyi wote, Malaika, Wa mbinguni mtaitika.

4 Manabii na Mababu, Mwone jambo la ajabu.

5 Nye Mitume na Wenjili, Tukuzeni fumbo hili.

6 Mashahidi, Waungama, Jongeeni kutazama.

 

Ewe Mwili wa Mwokozi

1 Ewe Mwili wa Mwokozi, Tunakusalimu. Umeteswa msalabani, Kwa ajili yetu.

Kiitikio: Tuabudu, tushukuru Kwa mapendo hayo- Kweli, tumependwa mno

2 Tusalimu pia Damu, Aliyomwagia. Ndiyo bei ya wokovu na fidia bora.

3 Heri sisi binadamu, twajaliwa sana. Mungu yuko kati yetu nasi tu salama.

 

Sakramenti Kubwa hiyo

Sakramenti kubwa hiyo, twaheshimu kifudi

Na sheria ya zamani ikomeshwe na hiyo,

Yafichikayo machoni imani huyaona.

 

Mungu Baba, Mungu Mwana asifiwe kwa shangwe,

Atukuzwe, ‘heshimiwe, pia aabudiwe;

Mungu Roho Mtakatifu vile sifa apate. Amina.

 

 1. Umewapa mkate utokao mbinguni (aleluya)
 2. Wenye utamu wa kila namna (aleluya)

 

Atukuzwe Mungu

1 Atukuzwe Mungu.

2 Litukuzwe Jina lake takatifu.

3 Atukuzwe Yesu Kristu, Mungu kweli na mtu kweli.

4 Litukuzwe Jina la Yesu.

5 Utukuzwe Moyo wake mtakatifu.

6 Itukuzwe Damu yake takatifu.

7 Atukuzwe Yesu katika Sakramenti takatifu ya altare.

8 Atukuzwe Roho Mtakatifu Mfariji.

9 Atukuzwe Mama wa Mungu, Maria mtakatifu.

10 Atukuzwe Maria aliyekingiwa dhambi ya asili.

11 Atukuzwe Maria aliyepalizwa mbinguni.

12 Litukuzwe Jina la Maria, Bikira na Mama.

13 Atukuzwe Mtakatifu Yosef, mchumba wake mwenye usafi kamili.

14 Atukuzwe Mungu katika malaika wake na watakatifu wake.

 

Tuiiabudu siku zote, Ekaristi Takatifu

 

Twakuomba Mama Maria

 1. Mama Maria Mwombezi wetu, Mama wa Neema na huruma/ tusikilize mama wa Yesu, tusikilize wakosefu.

Kiitikio:  Twakuomba Mama Maria kwa Mwanao Mama tuombee, Sala zetu Mama Maria kwa Mwanao

                 Mama zifikishe. Nyoyo zetu Mama Maria zatamani kufika mbinguni.

 1. Mama Maria uliye mwema, tuliza nyoyo zetu wanao/ Tunaposhindwa tusaidie, tusije baki katika giza.
 2. Mama Maria twakuamini, Mama wa Mungu msaada wetu/ Matumaini yetu ni kwako, katika shida tusimamie.
 3. Mama Maria usituache, umpelekee Bwana maombi/ atubariki wenye mashaka, tupate uzima wa milele.

 

FUNGU LA II

 

Binadamu inama Kichwa

 

 

 1. Binadamu inama Kichwa,

Umwabudie Mwokozi.

Hapa yupo, ajapofichwa;

Ameshuka chini kwetu!

 

 1. Kwa macho yetu hatuoni,

Ila maumbo ya mkate:

Hakuna ‘ta mkate lakini,

Mwiliwe twakiri sote.

 

 1. Kukaa nasi umetaka,

Rabi mwema, mpenda watu;

Kwa tamaa nyoyo zawaka:

Njoo basi,shuka kwetu!

 

 

Aleluya tumwabudu Yesu Kristu

 

 

Kiitikio: Aleluya tumwabudu Yesu Kristu

            Yu hai mzima katika Ekaristi

            Aleluya, Aleluya, Aleluya.

 

 1. Sakramenti hii kuu ya mapendo,

Alimojiweka Kwa’jili ya watu,

Nasi twakupa yetu leo mapendo.

 

 1. Ni sadaka ya msalaba twaijua,

Kafufuka kisha kapaa kwa Baba,

Yuko nasi katika hii Ekaristi.

 

 1. Ni chakula chetu bora na kwa roho,

Ni Mwanakondoo yule wa Pasaka,

Atulisha atushibisha daima.

 

 1. Njoni wote tumwabudu Yesu Kristu,

Nyoyo zetu nyimbo zetu tumtolee,

Sifa zetu shangwe zetu tumpatie.

 

 1. Mwili wako uwe asili ya heri,

Utakase nyoyo zetu kwa damuyo,

Zifike mbinguni daima milele.

 

 

Sakramenti Kubwa Hiyo  (Tantum ergo)

 

Sakramenti kubwa hiyo, twaheshimu kifudi;

Na sheria ya zamani ikomeshwe na hiyo,

Yafichikayo machoni imani huyaona.

 

Mungu Baba, Mungu Mwana  asifiwe kwa shangwe,

Atukuzwe, 'heshimiwe, pia aabudiwe;

Mungu Roho Mtakatifu vile sifa apate. Amina.

 

Tantum ergo Sacramentum,  Venerernur cernui:

Et antiquum documentum,  Novo cedat ritui:

Praestet fides supplementum,  Sensuum defectui.

 

Genitöri, Genitöque,  Laus et iubilätio:

Salus, honor, virtus quoque,  Sit et benedictio;

Procedenti ab utröque,  Compar sit Iaudätio. Amen.

 

 1. K. Umewapa mkate utokao mbinguni (aleluya).
 2. Wenye nguvu ya kufurahisha wote (aleluya).

Kisha Baraka ya Sakramenti Takatifu

 

 

Kiitikio: Atukuzwe Mungu wetu pote daima.

 

 1. Tukuzeni Mungu,

Enyi viumbe vya dunia na mbingu.

Litukuzeni jina lake.

 

 1. Tukuzeni Yesu,

Mungu mkombozi wetu mwenye huruma.

Ashangiliwe hapa petu.

 

 1. Tukuzeni damu ya Yesu,

Bora sana kwa binadamu.

Tumpe shukrani kwa memaye.

 

 1. Tukuzeni mwili wa Yesu,

Sakramenti yake tukufu.

Tumpe heshima altareni.

 

 1. Tukuzeni Mama wa Yesu Kristu,

Mama wa Mungu  wetu.

Yeye ni Mama na Bikira.

 

 

Kristu Mshinda, Kristu Mfalme, Kristu Kristu Mtawala

Christus Vincit, Christus Regnat, Christus, Christus Imperat.

 

 

Kweli nakuamini Maria Bikira

 

1 Kweli nakuamini, Maria Bikira:

Po pote duniani, Uwe mlinzi bora:

Siku yo yote kwako Nikiomba mema,

Sinitupe mja wako, Kwani wangu Mama.

 

2 Ni wako Yesu Mwana, Kwake nisemee,

Niepuke laana. Nisipotelee!

            lfikie uwingu Sala nisaliyo;

Umpelekee Mungu, Asifumbe moyo.

 

3 Sinache saa ile Pumzi nikikata.

Namchea Mwamzi yule, Nisitiwe matata:

Ee Mama wangu mwema Unisimamie,

Hatima kifo chema Mwisho nipatie!

 

Tuna Mama uwinguni

I.Tuna Mama uwinguni, Mama mwema sana, Tuliao taabuni, Ndi'si wake wana.

Kiitikio: Mama wetu mwema, mtamu, Jina lake ni Maria.

Ewe Mama, tufahamu, Kwani twasumbuka mno.

 1. Tuna Mama mpendelevu Mwingi wa rehema. Hupokea wapotevu Hugawia mema.
 2. Tuna Mama mwaminifu, Mlinzi hatarini. Mnyonge, mkiwa na dhaifu Bure hamwamini.
 3. Tuna Mama na mwombezi, Lote awezalo. Hupatia kwa Mwenyezi Kila aombalo.

 

 

FUNGU III

Viumbe nyi  vya Dunia

1 Viumbe nyi vya dunia Na vya mbingu njoni!

Sogeeni kuangalia, Hapa kuna nini!

Ndiyo Kuu Sakramenti, Ni Yesu wa Ekaristi;

Twende mwabudia Chini ya Hostia.

2 Wa Malaika Malkia, Njoo shuka kwetu;

Mwabudia, mwangukia, Mwanao Mungu Mtu!

ututie shime Mama, Tuweze mpenda daima;

Leo duniani, Kesho uwinguni!

3 Enyi pia Malaika, Wakazi wa juu,

Jongeeni kwa furaha Kuimbia mkate huu!

Mitume na Manabii, Mabikira, Mashahidi,

Nanyi karibuni, Yesu mtukuzeni!

4 Twende nasi masikini Mwangukia Yesu

Ni mpenzi wetu amini Mlo wa roho zetu!

Kwake heri hapa chini, Kwake raha uwinguni!

Asifiwe pote, Na viumbe vyote!

 

Tupalize sauti zetu

1 Tupalize sauti zetu, Wote tumtukuze leo.

Tumtukuze Mwokozi wetu, Mpenda ya kwetu makao.

Yesu, ndiwe mchungaji  mwema, Twakuja siye wakristu;

Zipokee zetu heshima, Zipokee nyoyo zetu.

2 Wazee wetu wa zamani, Sadaka nao hutoa,

Wakifukizia ubani, Na nyama wakichinjia.

Mara katokea Mwokozi: "Acheni kondoo mbali.

Baba yangu hazimpendezi; Ndimi sadaka ya kweli »

3 Isipomtosha msalabani Mara moja atolewe,

Akatwaa mkate mezani, Kaugeuza mwiliwe;

"Mle, huu ndio mwili wangu» Mitume kiwaambia.

Ndiyo sadaka mpya ya Mungu, Nda peke kutufalia.

4 Basi, Mitume tangu hapo Hutoa sadaka ile,

Miji na nchi wapitiapo, Kumkumbuka Rabi vile.

Hata leo kwetu mijini, Padre hutoa sadaka,

Yesu hutoka uwinguni, Mpenda kwa watu kushuka.

5 Yesu, Mkombozi kwa damuyo, Wala hukutusahao

Siye, watu wa bara hiyo, Ukatutokea leo!

Mungu pamwe na binadamu, Mtu Mungu twakuungama;

Twaabudu mwili na damu, Kichwa chini tukiinama.

 

Sakramenti Kubwa hiyo

Sakramenti kubwa hiyo, twaheshimu kifudi

Na sheria ya zamani ikomeshwe na hiyo,

Yafichikayo machoni imani huyaona.

Mungu Baba, Mungu Mwana asifiwe kwa shangwe,

Atukuzwe, ‘heshimiwe, pia aabudiwe;

Mungu Roho Mtakatifu vile sifa apate. Amina.

 

 

 1. Umewapa mkate utokao mbinguni (aleluya)
 2. Wenye utamu wa kila namna (aleluya)

 

Atukuzwe Mungu

1 Atukuzwe Mungu.

2 Litukuzwe Jina lake takatifu.

3 Atukuzwe Yesu Kristu, Mungu kweli na mtu kweli.

4 Litukuzwe Jina la Yesu.

5 Utukuzwe Moyo wake mtakatifu.

6 Itukuzwe Damu yake takatifu.

7 Atukuzwe Yesu katika Sakramenti takatifu ya altare.

8 Atukuzwe Roho Mtakatifu Mfariji.

9 Atukuzwe Mama wa Mungu, Maria mtakatifu.

10 Atukuzwe Maria aliyekingiwa dhambi ya asili.

11 Atukuzwe Maria aliyepalizwa mbinguni.

12 Litukuzwe Jina la Maria, Bikira na Mama.

13 Atukuzwe Mtakatifu Yosef, mchumba wake mwenye usafi kamili.

14 Atukuzwe Mungu katika malaika wake na watakatifu wake.

 

  Tuiiabudu siku zote, Ekaristi Takatifu

 

Siku zote tuimbe sote

 1. Siku zote Tuimbe sote Sifa zake Maria. Tumwendee, Tumtolee, Na nyimbo na salamu.   

Mpende    vema, Ana neema, Ni Bikira mtukufu. Umwendee, Umlilie, Saa ya usumbufu.

 

 1. Amwazaye, Amwombaye, Mtu huyo ni salama: Hujiliwa, Huinuliwa, Hujua ana Mama.

Mama juu, Mweza mkuu, Usoni kwa Mwanaye, Amsalia, Amwombea, Mungu asikatae.

 

 1. Tutendeje, Tufanyeje, Tumshukuru Bikira? Yesu mpenzi, Mkombozi, Tumtii barabara;

            Yake shauri, Hasa amri, Na mafundisho yake, Kusikiza, Kutimiza, Mwisho wetu tuokoke!

 

 

IV

NYIMBO ZA KUABUDU SAKRAMENTI KUU (BARAKA).

TUMWABUDU YESU.

Tumwabudu Ye-su, //chini ya maumbo ha-ya, ya mkate na divai ya-ke //x2

 1. Yesu kasema, huu mwili wangu, Yesu kasema, hii damu ya-ngu.
 2. Kwa mwili wako, unatushibisha, watupa afya, ya mwili na roho.
 3. Kwa damu yako, watuliza kiu, wachangamsha, furaha ya mbingu.
 4. Twakuabudu, ewe Yesu mwema, tawala roho, na mawazo ye-tu.
 5. Mwili na damu, unatushibisha, mema ya Mbingu, hapa dunia-ni.
 6. Ee Yesu mwema, watupenda sana, utufikishe, kule juu mbingu-ni.

 note

TUMWANGUKIE YESU NA MOYO WAKE MKUU

Tumwangukie Yesu na Moyo wake mkuu x2// Tumpende tumshukuru milele tumsifu x2

 1. (I,ii) Kuliko nyoyo zote ni mmoja moyo mkuu, mapendo yake kwetu hayana kifani // Tumpende tumshukuru milele tumsifu x2
 2. Ee Moyo wa huruma wa Yesu mkombozi, umetupa wokovu kwa kufa mtini. // Tumpende tumshukuru milele tumsifu x2
 3. Kisima cha furaha na cha fara-ja kuu, tukitamani Roho tuje ku-teka tuu. // Tumpende tumshukuru milele tumsifu x2

 

LITANIA YA MOYO MTAKATIFU WA YESU.

(kiitikio wote)

Moyo Mtakatifu wa Mwokozi Yesu Kristo ((i) Moyo wake Ye-su) uliofunuliwa kwa Mku-ki, utujalie wokovu Mungu we-tu.

 1. Mo-yo wake Yesu, Mwa-na wake Ba-ba, Ba-ba wa milele/ Mo-yo ulotungwa, na Roho Mtakatifu mwili-ni mwa Bikira, utuhurumie.
 2. Mo-yo wake Yesu, uliounga-na na Ne-no wa Mungu/ Mo-yo wake Yesu, ulio na Utukufu pa-sipo m-fano, utuhurumie.
 3. Mo-yo wake Yesu, he-kalu Ta-katifu la Mu-ngu/ Mo-yo wake Yesu, he-ma la Yu-le A-li-ye juu, utuhurumie,
 4. Mo-yo wake Yesu, nyu-mba ya Mu-ngu na Mla-ngo wa mbinguni/ Mo-yo wake Yesu, ta-nuru ye-nye, kuwa-ka ma-pendo, utuhurumie.

(Kiitikio wote)

________________________________

 1. Mo-yo wake Yesu, cho-mbo cha ha-ki, na cho-mbo cha mapendo/ Mo-yo wake Yesu, u-naoja-a upe-ndo na wema, utuhurumie
 2. Mo-yo wake Yesu, Mo-yo ni ki-lindi cha fa-dhila zote/ Mo-yo wake Yesu, u-naosta-hi-li si-fa zote, utuhurumie.
 3. Mo-yo wake Yesu, u-naota-wala mi-o-yo yote/ Mo-yo wake Yesu, zinamokaa hazina hekima na elimu, utuhurumie.
 4. Mo-yo wake Yesu, u-timili-fu wo-te wa Mungu/ Mo-yo wake Yesu, uliopendelewa kabi-sa na Mungu, utuhurumie.

 (kiitikio wote)

__________________________________

 1. Mo-yo wake Yesu, ulotuenezea mazi-a-da yake/ Mo-yo wake Yesu, mtamaniwa wa vilima vya mi-lele, utuhurumie.
 2. Mo-yowake Yesu, wenye uvumilivu na hu-ru-ma nyingi/ Mo-yo wake Yesu, ta-jiri kwa wo-te we-nye kukuomba, utuhurumie.

 3. Mo-yowake Yesu, chemchemi ya uzima na u-ta-katifu/ Mo-yo wake Yesu, ma-lipo kwa dha-mbi ze-tu wanadamu, utuhurumie.

 4. Mo-yowake Yesu, u-lioshi-bishwa sa-na kwa matusi/ Mo-yo wake Yesu, u-liovunjika kwa u-ba-ya wetu, utuhurumie.

(kiitikio wote)

____________________________________

 1. Mo-yowake Yesu, u-li-o-tii m-paka kufa/ Mo-yo wake Yesu, Mo-yo uli-ochomwa kwa m-kuki, utuhurumie.
 2. Mo-yowake Yesu, chem-chemi ya fa-ra-ja zote/ Mo-yo wake Yesu, u-zima nao u-fu-fu-o wetu, utuhurumie.
 3. Mo-yowake Yesu, a-mani na u-pata-nisho wetu/ Mo-yo wake Yesu, sa-daka ye-tu sisi wa-ko-sefu, utuhurumie.
 4. Mo-yowake Yesu, wo-kovu wa we-nye ku-kutumaini/ Mo-yo wake Yesu, tu-maini la-o we-nye kuzimia, utuhurumie.

(kiitikio wote)

____________________________________

 

 1. Mo-yowake Yesu, fu-raha ya Wa-taka-ti-fu wote/ Mo-yo wake Yesu, m-pole na m-nyenye-ke-vu kwetu, utuhurumie.
 2. Mo-yowake Yesu, u-ondoa-ye dhambi za ulimwengu/ Mo-yo wake Yesu, li-nganisha nyoyo zetu na Moyo wako, utuhurumie.

 3. EeMu-ngu Mwenyezi, u-uanga-li-e Mo-yo wa Mwanao/ Mo-yo wake Yesu, m-pendele-vu pia na he-shima, utuhurumie.
 4. Mo-yowa Mwanao, a-lojitolea malipo ya wenye dhambi/ Uwahurumie, we-nye kuku-omba toba ee Baba, utuhurumie.

(kiitikio wote)

note

SAKRAMENT KUBWA HIYO

Sakramenti kubwa hiyo, twaheshimu kifudi;

Na sheria ya zamani ikomeshwe na hiyo,

Yafichikayo machoni imani huyaona.

                  Mungu Baba, Mungu Mwana asifiwe kwa shangwe,

                  Atukuzwe, ‘heshimiwe, pia aabudiwe;

                  Mungu Roho Mtakatifu vile sifa apate. Amina.

 

ATUKUZWE MUNGU WETU MTAKATIFU.

 1. ((i)Atukuzwe Mungu wetu Mtaka-tifu) – Atukuzwe Mungu wetu Mtaka-tifu.
 2. Litukuzwe Jina lake Taka-tifu – Litukuzwe Jina lake Taka-tifu
 3. Atukuzwe Yesu Kristo Mungu na mtu – Atukuzwe Yesu Kristo Mungu na mtu
 4. Litukuzwe Jina lake taka-tifu – Litukuzwe Jina lake taka-tifu
 5. Utukuzwe Moyo wake mtaka-tifu – Utukuzwe Moyo wake mtaka-tifu
 6. Itukuzwe Damu yake taka-tifu – Itukuzwe Damu yake taka-tifu
 7. Atukuzwe Roho Mtakatifu Mfariji – Atukuzwe Roho Mtakatifu Mfariji
 8. Atukuzwe Yesu katika Sakramenti – Atukuzwe Yesu katika Sakramenti
 9. Atukuzwe Maria mama wa Mungu – Atukuzwe Maria mama wa Mungu
 10. Atukuzwe Maria aliyekingiwa –Atukuzwe Maria aliyekingiwa
 11. Atukuzwe Maria aliyepalizwa –Atukuzwe Maria aliyepalizwa
 12. Litukuzwe jina la Bikira na mama –Litukuzwe jina la Bikira na mama
 13. Atukuzwe Yosefu wa usafi kamili – Atukuzwe Yosefu wa usafi kamili
 14. Atukuzwe Mungu katika wateule -Atukuzwe Mungu katika wateule

note 

SIFA NA SHUKRANI

((i)Sifa na shukrani) ziwe siku zote, kwa sakramenti takatifu mno ya Mu-ngu.

- Msifuni Bwana enye mataifa yo-te, msifuni enyi makabila yote.

- Maana huruma yake ni daima kwe-tu, na uaminifu wa Bwana ni wa milele.

- Atukuzwe Baba na mwa-na, na Roho Mtakatifu,

- Kama mwanzo na sasa na siku zo-te, na milele Amina.

 

NITAIMBA SIKU ZOTE WA YESU MOYO MKUU

Nitaimba siku zote wa Yesu Moyo Mkuu, kuliko vitu vyote nitapenda moyo huu. x2

 1. Ee Moyo Mtakatifu wa Yesu wangu, nakuja kukusifu kwa hizo nyimbo zangu.
 2. Kwa nini nikapenda furaha za dunia, kwa nini sikwenda kwa Yesu kutulia.
 3. Ee Yesu wangu mwema Mtakatifu, unipe moyo wako niweze kukusifu.

 

Pin It