BWANA WETU YESU KRISTU MFALME
ASTAHILI ENZI
Astahili enzi utajiri na heshima, milele milele milele mile-le x2.
1. Mwanakondoo aliyechinjwa, astahili kupokea uweza, utajiri, hekima, nguvu na heshima.
2. Utukufu na ukuu una Yeye, hata milele na milele.
BWANA NI MFALME
(iv Bwana ni mfalme) Bwana ni mfalme, //amejivika jivika Taji (iv Bwana) amejivika jivika Taji.
1. Bwana ametamalaki, amejivika adhama/ Bwana amejivika na kujikaza nguvu.
2. Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike; Kiti chako kimekuwa thabiti tokea zamani/ Wewe ndiwe uliye tangu milele.
3. Shuhuda zako ni amini sana; Utakatifu ndio uifaao nyumba yako/ Ee Bwana milele na milele.
BWANA MFALME AMEKETI MILELE.
Bwana mfalme ameketi milele, atawabariki watu kwa amani x2
1. Atawala, duniani na mbinguni, toka mto hata kingo za dunia.
2. Na wafalme, wote watamwabudia, mataifa yote watamtumikia.
3. Na ufalme, wake wadumu milele, ni ufalme mkuu usio na mwisho.
PENTEKOSTE
TWAKUOMBA UJE ROHO
Twakuomba uje Roho Mfariji –Uje Roho Mtakatifu mfariji
Twakuomba uje kutufariji – Uje Roho Mtakatifu mfariji.
//Nyoyo zetu ni altare ya-ko, uzipambe kwa mapaji ya-ko, uje roho Mtakatifu mfariji x2.
1. Utujazi na mapaji yako – Uje Roho ..../ Tufundishwe naye Roho wako – Uje Roho ...
2. Roho wako ndiye mleta mapaji – Uje .../ Bila yeye hatuwezi fahamu – Uje ...
WAIPELEKA ROHO YAKO (Pd. Richard Kimbwi)
Waipeleka Roho yako ee Bwana, nawe waufanya upya uso wan chi x2
1. Ewe nafsi yangu umhimidi Bwana, wewe Bwana Mungu wangu mkuu sana.
2. Ee Bwana ninsi yalivyo matendo yako, nchi yote imejaa ma-li zako.
3. Waondoa pumzi yao wanaokufa, na kuyarudia kweli mavumbi yao.
ROHO WA BWANA
Roho wa Bwana kaujaza ulimwengu, yeye aliye na mambo yo-te x2
1. Roho wa Bwana tuliyepe-wa, atafundisha mambo yo-te.
2. Uwashe ndani yetu si-si, ule moto wa pendo la-ko.
3. Roho Mtakatifu mfari-ji, ndiye tuliyepewa si-si.
KUKAJA UPEPO
Kukaja upepo kutoka mbinguni juu, na wote wakajazwa na Roho Mtakatifu x2
1. Naye aliye na mambo yote ndani mwa-ke/ anaujuzi wa kila neno aleluya.
2. Waipeleka Roho wako ee Bwa-na/ nawe wa ufanya upya uso wa nchi aleluya.
3. Pendo la Mungu limekwisha kumimi-nwa/ katika mioyo yetu aleluya.
4. Roho Mtakatifu tuliyepewa si-si/ anaujuzi wa kila neno aleluya.
UTATU MTAKATIFU
USIFIWE UTATU MTAKATIFU
(I, Usifiwe) Utatu Mtakati – fu, (I, Na umoja) usio gawanyika x2.
1. Asifiwe Mungu Baba na Mwana na Roho Mtakati – fu// kwa sababu ametufanyizia huruma yake.
2. Mungu Baba Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakati – fu// ni Nafsi tatu katika Mungu Mmoja.
3. Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakati – fu// kama mwanzo na sasa na siku zote na milele Amina.
WASTAHILI KUSIFIWA
Wa – stahili, ku – sifiwa, /: na kutukuzwa mile – le :/ x2.
1. Umehimidiwa, Mungu wa baba zetu, na kutuzwa milele.
2. Limehimidiwa, Jina lako tukufu, na kutuzwa milele.
3. Limehimidiwa, Hekalu Takatifu, na kutuzwa milele.
4. Umehimidiwa, kiti cha ufalme wako, na kutuzwa milele.