MIMI NI MTUMISHI WAKE BWANA
Mimi ni mtumishi wake Bwa – na, nitendewe ulivyo ne – na x2
Nitendewe (nitendewe) ulivyone-na (ulivyonena) mimi ni mtumishi wa Bwana (wa Bwana). Mimi nimtumishi wa Bwana. Nitende-we ulivyonena x2
1. Salamu Mariamu umejaa nee-ma/ Bwana yu pamoja nawe. Wewe umebarikiwa na Bwana/ kuliko wanawake wo-te.
2. Usiogope Maria-mu/ kwa maana umepata neema kwa Mungu. Tazama utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume/ na jina lake utamwita Yesu.
MARIA MWOMBEZI
Maria mwombezi, sisi wanawako katika shida yetu uliye kinga yetu (Maria) Twakuomba sana, tupe neema zako, tufike uwinguni uliko mama yetu.
1. Maria mama kimbilio letu, tupe msaada tuweze kushinda.
2. Katika vita yetu na shetani, tupe neema zako tusaidie.
BIKIRA MARIA.
(I: Bikira maria)mama wa Mungu kweli, ulizaliwa pasipo kuwa na dha-mbi x2
1. Hakuna mwanamke, mwi-ngine duniani, aliyebarikiwa kama ulivyo, twakusifu tunakuheshi-mu.
2. Malaika mbinguni wanasifu jina lako, na dunia pia tunalitaja utamu wa jina hauishi.
MAOMBIZI YAKO MARIA
Maombezi yako Maria kwa mwanao, yatupatia faraja siku zote x2
1. Sala zako Mari-a kwa Yesu Kristo, zatupa tumaini maishani mwetu. Fadhila zako Mama kwa Yesu Kristo, zatupa neema na wokovu siku zote.
2. Uzidi kutuombea mama mwema, ili tuweze shinda nguvu za shetani. Ulinzi wako mama kwa wana wako, watupa tumaini maishani mwetu.