MISA YA MAREHEMU
UWAPE EE BWANA RAHA YA MILELE
(I, Uwape ee Bwana) Raha ya milele (I,III mwanga wa milele) uwaangazie x2
1. Kama vile Kristo alivyokufa na kufufu---ka/ vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja na---ye.
2. Kwa kuwa katika Adamu wote wanaku---fa/ kadhalika na katika Kristo wote watahui---shwa.
3. Ee Mungu, wewe ndiwe utukufu wa waamini na uzima wa wenye ha---ki/ Mwanao amewakomboa kwa kifo na ufufuko wa---ke.
TUMAINI LETU NI KWA BWANA
Tumaini letu ni kwa Bwa---na, kwa maana ana uwezo wa milele x2
1. Tutamsifu Bwana siku zo---te, kwa maana ana uwezo wa milele.
2. Yeye ndiye mwanzo wa uzi---ma, kwa maana ana uwezo wa milele.
3. Yeye ndiye aliyetuumba, kwa maana ana uwezo wa milele.
4. Vitu vyote vimeumbwa na---ye, kwa maana ana uwezo wa milele.
5. Yeye ndiye kiongozi we---tu, kwa maana ana uwezo wa milele.
6. Tumwabudu tumsifu dai---ma, kwa maana ana uwezo wa milele.
ZAENI MATUNDA MEMA
1. Zaeni matunda me---ma, zaeni matunda ya---le, zaeni yenye bara---ka, zaeni ya heri:
Bwana akiyapoke---ya, yatabarikiwa vye---ma zaeni matunda me---ma, zaeni ya heri x2
2. Sarisha mwenendo wa---ko, safisha matendo ya---ko; safisha na Bwana Ye---su, safisha yo---te
3. Fanyeni kazhi kidu---gu, fanyeni kazi kwa bi---dii, fanyeni na Bwana Ye---su, fanyeni yo---te.
4. Tolea matunda ya---ko, pamoja na moyo wa---ko; naye Bwana Mungu wa---ko, atakubarikia.
5. Baraka za Mungu Ba---ba, Baraka za Mungu Mwa---na, na za Roho Mtakati---fu, ziwe nanyi nyote.
MIMI NDIMI UFUFUO NA UZIMA
Mimi ndimi ufufuo na uzima, yeye aniaminiye ajapokufa atakuwa anai---shi x2
1. Naye kila aishie na kuniami---ni/ hatakufa kabisa hata mile---le.
2. Kama Kristo alivyokufa akafufu---ka/ vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja na---ye.
3. Kwa kuwa kama katika Adamu wote wanaku---fa/ kadhalika na katika Kristo wote watahui---shwa.
KUABUDU
NAKWABUDU YESU:
1. Nakuabudu Yesu katika Hosti-ya, u Mungu kweli na mwanadamu katika sakramenti
(nakwabudu) nakwabudu fudifudi, ee mfalme mtukufu wa milele.
2. Ee Yesu, kwa mapendo unakaa kwetu, u mgeni wetu toka mbinguni, twakuja kuabudu.
3. Baraka yako, Yesu utupatie, tukinge na maovu ya leo, tuishi kwa amani.
4. Uwabariki pia wapenzi wetu, uwajalie neema yako, watoe shukrani kuu.
SAKRAMENTI KUBWA HIYO
1. Sakramenti kubwa hiyo, twaheshimu kifudi, na sharia ya zamani ikomeshwe na hiyo, yafichikayo machoni imani hu-ya-o-na.
2. Mungu baba Mungu Mwa-na asifiwe kwa shangwe; kwa heshima atukuzwe, pia aabudiwe, Mungu Roho Mtakatifu vile sifa a-pate. A-mina
ATUKUZWE MUNGU -
Atukuzwe Mu-ngu, litukuzwe Jina lake Takati-fu /Atukuzwe Yesu Kri-sto, Mungu kweli na mtu kweli.
- Litukuzwe Jina la Ye-su, utukuzwe Moyo wake mtakati-fu/ Itukuzwe Da-mu, yake takatifu.
- Atukuzwe Ye-su, katika Sakramenti takatifu ya Alta-re/ Atukuzwe Ro-ho, Mtakatifu mfari-ji.
- Atukuzwe mama wa Mu-ngu, Maria mtakati-fu/ Atukuzwe Mari-a, aliyekingiwa dhambi ya asili.
- Atukuzwe Mari-a, aliyepalizwa mbingu-ni/ litukuzwe jina la Mari-a, Bikira na Mama.
- Atukuzwe Mtakatifu Yose-fu, mume wake mwenye usafi kami-li/ atukuzwe Mu-ngu, katika malaika na watakatifu wake.
KRISTU MSHINDA
Kristu mshinda Kristu mfalme, Kristu Kristo mtawala.
1. Baba Mtakatifu wetu, Frasisko, makadinari na ma – skofu wetu, tunawaombea Baraka na afya nje-ma.
2. Tujaliwe afya nje-ma, amani ya Kristo i-je, utawala wa Mungu ufike.
NINAKUABUDU MUNGU WANGU
1. Ninakuabudu Mungu wangu, unayejificha altareni; ninakutolea moyo wangu, usiofahamu siri yako.
2. Mafahamu yangu yadanganya, yanapokuona na kugusa; namsadiki Yesu, hadanganyi, yeye Mungu Mwana na ukweli.
3. Waficha umungu msalabani, na ubinadamu altareni; nami naungama zote mbili kama mwivi yule mwenye toba.
4. Tomas aligusa majeraha, nami nasadiki bila shaka; ewe Ye-su nipe pendo lako, tumaini kwako na imani.
5. Umeteswa nini, Bwana mwema, kwa kunipa mkate wa uzima?; Yesu unifiche, ndani yako, ili nilionje pendo lako.
6. Yesu pelikane, nitazame, na kwa damu yako nitakase; tone moja ndilo linatosha , na dunia yote yaokoka.
7. Ndani ya mafumbo Yesu yumo, Atafumbuliwa kwangu lini; nikuone Yesu, uso wako, nishiriki nawe heri yako. A-mina
NDOA
NIMEINGIA HAPA MAHALI
Nimeingia (kwako) hapa mahali patakatifu Unipokee (Bwana) unitakase nipate neema.
1. Uwapokee Bwana watumishi wako, wanaokuja kufunga ndoa
2. Upendo wako Bwana uwatawale, maisha yao mapya ya ndoa
3. Uwajalie upendo maishani, ndoa idumu maisha yote
FADHILI ZA BWANA
Fadhili za Bwana zina wamchao, tangu milele hata milele x2
1. Tazama mke wako atakuwa kama mdhabibu/ wenye kuzaa matunda mema.
2. Mungu alimpatia Adamu mke ili awe msaidizi na tegemeo lake/ na kwao umetoka uzao wote wa wanadamu.
3. Kwa sakramenti ya ndoa nyingi mtakuwa mwili mmoja/ muishi kwa umoja na upendo
TWAKUSHUKURU EE BWANA.
Twakushukuru ee Bwana muumba wa vyote, asante kwa wanawako walofunga ndoa x2
1. Umewaleta hapa, kuwaunganisha, kwa maisha mapya ya ndoa na familiya/ umewaleta hapa, waoneshe pendo, lilokati yao na wewe Mungu mwenyezi.
2. Tunawaombea, kwako Mungu Baba, waishi maisha mema na yenye upendo/ Furaha yao Bwana, kukutumikia, wajalie watoto wema wenye upendo.
NYINGINEZO
TUMWANGUKIE YESU NA MOYO WAKE MKUU
Tumwangukie Yesu na Moyo wake mkuu x2// Tumpende tumshukuru milele tumsifu x2
1. (I,ii) Kuliko nyoyo zote ni mmoja moyo mkuu, mapendo yake kwetu hayana kifani // Tumpende tumshukuru milele tumsifu x2
2. Ee Moyo wa huruma wa Yesu mkombozi, umetupa wokovu kwa kufa mtini. // Tumpende tumshukuru milele tumsifu x2
3. Kisima cha furaha na cha fara-ja kuu, tukitamani Roho tuje ku-teka tuu. // Tumpende tumshukuru milele tumsifu x2