KWARESIMA
ATANIITA
Ataniita nami nitamwitikia, nitamwokoa na kumtukuza x2
1. Kwa siku nyingi nitamshibisha/ nitamwokoa na kumtukuza.
2. Ee Bwana utupe rehema zako/ ili tuyajue matendo mema ya mwanao
SAUTI YA BABA
Sauti ya Baba ilitoka katika wingu jeupe, huyu ni mwanangu mpendwa, ninaye pendezwa naye, msikieni yeye x2
a. Na wale wanafunzi waliposikia, walianguka kifulifuli, wakaogopa sana.
b. Yesu akaja akawagusa akawagusa akasema, inukeni, wala msiogope.
c. Wakainua macho yao wasione mtu, ila Yesu, Yesu peke yake.
Utukufu wa Msalaba
Kwa ishara ya msalaba tuokoe
1. Utukufu wa msalaba twaadhimu/ wa msalaba wake Yesu, ulio uzima na fahari yetu.
2. Utukufu wa msalaba twaadhimu/ Juu yake Bwana Yesu, ametukomboa kwa kumwaga damu.
3. Utukufu wa msalaba twaadhimu/ Ju yake mti huo, Yesu alishinda enzi ya shetani.
4. Utukufu wa msalaba twaadhimu/ chombo cha mateso mengi, kugeuka chombo cha ushindi mkuu.
PASIPO MAKOSA
1. Pasipo makosa mkombozi wetu, katika baraza ya wakosefu, na wote walia asulubiwe, //aachwe Baraba na Yesu afe//x2
2. Ee Yesu, washika msalaba wako, na unakubali kufa juu yake. Ee Yesu useme sababu gani // ya nini mateso makali hayo//x2
3. Ni pendo la Baba wa uwinguni, ni huruma yake kwa wakosefu. We mkristu, kumbuka mateso yangu, // uache makosa, uache dhambi//x2
MTU HATAISHI KWA MKATE.
((I) Mtu hataishi kwa mkate) mtu hataishi kwa mkate, kwa mkate peke yake ((ii) i-la)
//ila kwa kila neno litokalo kinywani mwa Mungu// x2
1. Nawe uzishike amri za Bwana, upate kwenda katika njia zake Bwana.
2. Bwana ni mkate ule wa uzima, tumpokee tupate neema za mbinguni.
3. Bwana ni uzima wa mwili na Roho, anashibisha Roho na mema ya mbinguni.
4. Bwana atupenda sisi watu wake, tujitakase kweli kwa toba na mfungo.
note
MAMA PALE MSALABANI
Mama pa-le msalabani, macho ya toka machozi x2
1. Mwone vile akilia uchungu kama upanga, ukampenya moyowe.
2. Mwenye moyo mgumu nani asimuhurumie basi, mama mlilia mwanawe.
note
JUMAPILI YA MATAWI
HOSANA KWA MWANA WA DAUDI.
((i)Hosana kwa mwana) wa Daudi x2 Hosana kwa mwana wa Daudi x2.
a. Mbarikiwa yeye ajaye/ kwa jina lake Daudi.
b. Yeye ndiye Mbarikiwa/ na mfalme wetu na mrithi wake Daudi.
c. Mungu ndiye mfalme wa dunia yote/ Imbeni kwa akili.
YESU ALIPOINGIA MJI MTAKATIFU(frt. R.Kimbwi)
Yesu alipoingia mji mtakatifu, walitangaza ufufuko wa uzima x2
a. Walipaaza sauti wakiwa na matawi ya mitene/ wakasema Hosana juu mbinguni.
note
WATU WALIOPOSIKA YESU ANAKUJA (frt. Richard Kimbwi)
Watu waliposikia (iv yakuwa) Yesu anakuja, Yerusalemu walitoka kwenda kumlaki.
1. Walizipaza sauti, wakiwa na matawi, ya mitende wakasema, Hosana juu mbinguni.
2. Wao walikuimbia, kabla hujateswa, na sisi tunakuimbia, unapotawala.
3. Ewe Bwana mfalme wetu, mwe-ma na mpole, twakusifu wewe Bwana, milele na milele.
note
PASAKA
NIMEFUFUKA.
Nimefufuka ni ngali pamoja nawe, umeniwekea mkono wa-ko // maarifa hayo ni ya ajabu aleluya//x2
1. Umenichunguza, mbele na nyuma, umeelewa na kwenda kwangu/ wewe waijua, kura yangu mimi, wewe wajua mtima wangu.
2. Tufurahi sote, Bwana kafufuka, mwovu shetani amemshinda/ Ukombozi wetu, sasa ni wazi, mwokozi Yesu katukomboa.
NIMEONA MAJI (Dec. Richard Kimbwi)
Nimeona maji yakitoka Hekaluni, upande wa kuume Aleluya x2
1. Nao watu wote waliofikiwa na maji hayo wataokoka, aleluya.
2. Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu Milele yote aleluya.
NJONI WEPENZI TUFANYE SHANGWE
Njoni wapenzi tufanye shangwe// Mwokozi Bwana amefufuka Viumbe vyote tufanye shangwe// Mwokozi Bwana amefufuka x2
1. Walinzi wake walishituka ---, wakawa kama wamezimia---
2. Kwa ufufuko wako, ee Bwana---, umeturudishia uzima---
3. Umewashinda adui zetu---, mauti kali, pia shetani---
4. Enzi ni yako ya umilele---, shukrani, sifa na utukufu---
SIKU HII NDIYO
Siku hii ndiyo aliyoifanya Bwana, tutashangilia na kuifurahia x2
1. Aleluya, Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema, kwa maana fadhili zake ni za milele/ Israel na aseme sasa, ya kwamba fadhili zake ni za milele.
2. Mkono wa kuume wa Bwana umetukuzwa, Mkono wa kuume wa Bwana hutenda makuu/ Sitakufa bali nitaishi, name nitayasimulia matendo ya Bwana.
3. Jiwe walilolikataa waashi, limekuwa jiwe kuu la pembeni/ Neno hili limetoka kwa Bwana, Nalo ni ajabu machoni petu.
SEKWENSIA.
Kristo Paska yetu amechinjwa sadaka, tuile karamuye na twimbe aleluya.
1. Aliyejitoa, sadaka ya Paska, wakristu wamtolee, sadaka ya sifa. Mwanakondoo amewakomboa kondoo, Kristu asiye na dhambi, ametupatanisha na Baba, watu wenye dhambi.
2. Mauti na uzima, vimeshindana ajabu, Mkuu wa uzima aliyekufa, atawala mzima. Utuambie Maria, uliona nini njiani, niliona kaburi la Kristu mzima, na utukufu wa mwenye aliyefufuka.
3. Mashahidi ni malaika, leso ya uso na mavazi, Kristu tumaini langu kafufuka, atawatangulia Galilaya. Twajua Kristu amefufuka kweli katika wafu, ewe Mfalme mshindaji, utuhurumie, Amina aleluya.
KAFUFUKA BWANA
Kafufuka Bwana Mwokozi we-tu x2 Tumshangilie Bwan kafufuka x2
1. A-mefufuka Bwana – tumshangilie Bwana kafufuka Tupige vigelegele - Tumshangilie Bwana kafufuka
2. Tuimbe na kucheza – Tumshangilie--- Ameyashinda mauti – Tumshangilie---
3. Ametoka mautini – Tumshangilie--- Sasa tumekombolewa – Tumshangilie---
BWANA YESU KAFUFUKA.
Bwana Yesu kafufuka, tumwimbie kwa furaha aleluya/ aleluya aleluya, aleluya aleluya, aleluya.
1. Kweli Yesu kafufuka/ asubuhi na mapema – aleluya
2. Kaburini ametoka/ vile alivyoagua – aleluya
3. Ameishinda mauti/ amemshinda shetani – aleluya
4. Mbingu umefunguliwa/ uzima umerudishwa – aleluya
5. Sitakufa nitaishi/ kutaja sifa za Bwana – aleluya
6. Ewe Yesu mshindaji/ utuhurumie sisi – aleluya
7. Shukrani kwa Mungu wetu/ kwa kuwa yeye ni mwema - aleluya
YESU MWANA WA MUNGU:
Yesu Mwana wa Mungu (x2), leo amefufuka Piga vigelegele (x2), leo amefufuka.
1. Yesu Mwana wa Mungu, kweli amefufuka/ Ahadi yatimia, mzima amefufuka.
2. Kristu mshindaji mkubwa, kweli amefufuka/ na Babaye mbinguni, kwa damuye azizi.
3. Kristu Mwana-kondoo, amechinjwa sadaka/ tu-ile karamuye, tuimbe aleluya.
4. Kristu mchungaji mwema, alitoa maisha/ kwa ajili ya kondoo, mzima amefufuka.