Like our Page

Yaliyopo

 

Retreat at Pfarre Gartenstadt

Dear St. Bakhita Community members,

We are all invited to a retreat @ Galvanigasse 1-3, 1210 Wien.

On 16 & 17th March 2018.

Friday: 18:00 - 20:00

Saturday: 9:00 - 20:00hrs

Retreat Master: Fr Nicholas Chileshe from Zambia.Talks will be in English and translated into Germany.All are welcome

**********

For More Details: www-gartenstadt.at

 

MUNGU BABA POKEA

1. Mungu Baba, pokea sadaka yetu leo, twakutoleayo kwa jina la Mwanao; Ya Abel na Ibrahimu ilikupendeza, yetu Baba ipendeze, upokee tu;

Upokee – sadaka yetu Ndilo fumbo – la kukupendeza // la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu// x2

2. Njoni wote tutoe sadaka yetu leo, kwa sifa na utukuru wake Mwenyezi. Mkate huu na divai viwe mwili wake, kwa heshima kuu sadaka tumtolee.

3. Ee Mwenyezi tupokee tuwe mali yako, twakusihi kwa shukrani kuu tupokee. Tunakutolea nguvu, kazi na mavuno, kwa huruma yako dhambi tuondolee.

4. Kama mwanzo Mungu baba nasi asifiwe, na Mwanaye ndiye aliyetukomboa; Roho Mtakatifu ndiye wetu mfariji, Tatu Mtakatifu, Mungu mmoja twakiri.

 

VITU VYOTE NI VYAKO

Vitu vyote ee Bwana ni mali yako, twavileta kwako x2

1. Mkate na Divai ee Bwana, tunakutolea upokee.

2. Twakuomba Bwana uzipokee, na sala zetu tunazotoa.

3. Tunakutolea na fedha zetu, mapato yetu ya wiki hii.

4. Tunajitolea sisi wenyewe, kwani Baba sote mali yako.

5. Tunakutolea maisha yetu, tupe neema kwa upendo wako.

 

TOA NDUGU

Toa ndugu toa ndugu x2 ulicho nacho wewe, Bwana anakuona mpaka moyoni mwako.

1. Sasa ndio wakati wa kutoa sadaka, kila mtu aanze kujifikiria.

2. Wiki nzima Bwana Mungu alikulinda vema, sasa nawe ndugu yangu ujifikirie.

3. Kumbuka jinsi Yesu alivyojitolea pale msalabani kwa ajili yetu.

4. Tolea moyo wako, pia matendo yako, naye Bwana Mungu akubarikie.

5. Baraka zake Mungu, za Baba na za mwana, za Roho Mtakatifu zikae nanyi nyote.

 

DUNIA NA VYOTE NI MALI YA BWANA

Dunia na vyote, vilivyomo ni mali ya Bwana, Dunia na wote, wakaao ndani ya-ke x2

1. Maana ameifanya, misingi ya dunia, na vyote vilivyomo, ameviratibisha…

2. Bwa-na Mungu wetu, kaumba vitu vyote, na sisi wanadamu, ni mali yake Bwana…

3. Sasa ndio wakati, wa kumtolea Baba, vyote tulivyonavyo, na atatubariki…

4. Kumbuka jinsi Yesu, alivyojitolea, pale msalabani, kwa ajili yetu sisi…

5. Tolea moyo wako, pia matendo yako, na yeye Bwana Mungu, na atakubariki …

6. Baraka zake Mungu, za Baba na za Mwana, za Roho Mtakatifu, zikae nanyi nyote …

 

ZAENI MATUNDA MEMA

1. Zaeni matunda me---ma, zaeni matunda ya---le, zaeni yenye bara---ka, zaeni ya heri:

Bwana akiyapoke---ya, yatabarikiwa vye---ma zaeni matunda me---ma, zaeni ya heri x2

2. Sarisha mwenendo wa---ko, safisha matendo ya---ko; safisha na Bwana Ye---su, safisha yo---te

3. Fanyeni kazhi kidu---gu, fanyeni kazi kwa bi---dii, fanyeni na Bwana Ye---su, fanyeni yo---te.

4. Tolea matunda ya---ko, pamoja na moyo wa---ko; naye Bwana Mungu wa---ko, atakubarikia.

5. Baraka za Mungu Ba---ba, Baraka za Mungu Mwa---na, na za Roho Mtakati---fu, ziwe nanyi nyote.

sauti

 

Pin It