Like our Page

Yaliyopo

 

Retreat at Pfarre Gartenstadt

Dear St. Bakhita Community members,

We are all invited to a retreat @ Galvanigasse 1-3, 1210 Wien.

On 16 & 17th March 2018.

Friday: 18:00 - 20:00

Saturday: 9:00 - 20:00hrs

Retreat Master: Fr Nicholas Chileshe from Zambia.Talks will be in English and translated into Germany.All are welcome

**********

For More Details: www-gartenstadt.at

 

NIMEFURAHIWA SANA KWASABABU.(Frt. Richard Kimbwi)

Nimefurahiwa sana kwa sababu, tutakwenda nyumbani mwa Bwa-na

//(iv)- ni Bwana) wa mabwana tumwabudu (iv)- ni mfalme) wa wafalme tumwabudu //x2

1. Nyumba yake Bwana ni Takatifu, makao yake utukufu wake.

2. Tujongee mbele zake kwa shukrani, tumfanyie shangwe ndiye Mungu wetu.

 

TUMEINGIA NYUMBANI MWA BWANA (Richard Kimbwi)

Tumeingia nyumbani mwa Bwana, tumfanyie sifa na shangwe x2

1. Hii ndiyo nyumba yake Bwana, tujongee kwa furaha.

2. Hii ndiyo nyumba yake Bwana, tujongee kumwabudu.

3. Nyumba yake Bwana ni Takatifu, tujongee kwa ibada.

4. Mungu ndiye Baba muumba wetu, tujongee kumwabudu.

note

 

NIMEINGIA HAPA MAHALI. (F.A. Nyundo)

Nimeingia (kwako) hapa mahali patakatifu/ Unipokee (Bwana) unitakase nipate neema.

1. Ee Bwana Mungu wewe mfariji mwema, nakuja kwako kukuabudu.

2. Utupokee sisi watoto wako, utujalie mema ya mbingu.

3. Nakuja kwako Baba Mtukufu sana, nikuabudu kwa moyo wote.

4. Bila ya wewe mimi siwezi kitu, unijalie maisha mema.

 

MFANYIENI SHANGWE
Mfanyieni shangwe dunia yote, na mtumikieni kwa furaha x2.
1. Alituumba tuko - watu wake// Sisi ni kondoo wa – malisho ye.
2. Twende mbele za Bwana – kwa furaha// Yeye ni Mfalme wetu – tumwabudu.
3. Mtumikieni yeye – Muumba wetu// Sisi viumbe vyake – tumwabudu.

TAZAMA NIMEKUJA
Tazama nimekuja ee Bwana, kuyafanya mapenzi yako x2
1. Nalimngoja Bwana kwa sabu-ri/ Akaniinamia akakisikia kili-o change.
2. Akatika wimbo mpya kinywani mwa-ngu/ ndiyo sifa zake Mungu wetu.
3. Dhabihu na matoleo hukupendezwa na-zo/ Masikio yangu umeya-zibua.
4. Kafara na sadaka za dhambi hukuzita-ka/ Ndipo niliposema tazama ni-me-ku-ja.

NITAJONGEA ALTARE YA MUNGU (fr. G.Kayetta)
Nitajongea Altare ya Mungu, furaha yangu na heri yangu siku zote
Nitajongea Altare ya Mungu, furaha yangu na heri yangu siku zote

1. Mpigieni Bwana vigelegele enyi wenye ha-ki/ kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo.
2. Nafsi zetu zinamngoja Bwa-na/ yeye ndiye msaada wetu na ngao yetu.
3. Ee Bwana fadhili zako zikae na-si/ kama vile tulivyokungoja wewe.

NALIFURAHIA WALIPONIAMBIA (frt. Richard Kimbwi)

Nalifurahiwa waliponiambia (na twende), twende nyumbani mwa Bwana

// Miguu yetu imesimama, ndani ya malango (yako) ee Yerusalemu. x2

1. Ee Yerusalemu uliyojengwa, kama mji ulioshikamana.

2. Amani na iwe ndani yako, ewe mji mtakatifu sana.

3. Na salama iwe kati yako, Yerusalemu mji mtakatifu.

note

 

Pin It