Like our Page

Yaliyopo

 

Retreat at Pfarre Gartenstadt

Dear St. Bakhita Community members,

We are all invited to a retreat @ Galvanigasse 1-3, 1210 Wien.

On 16 & 17th March 2018.

Friday: 18:00 - 20:00

Saturday: 9:00 - 20:00hrs

Retreat Master: Fr Nicholas Chileshe from Zambia.Talks will be in English and translated into Germany.All are welcome

**********

For More Details: www-gartenstadt.at

 

NYIMBO KIPINDI CHA KWARESMA

JUMAPILI YA PILI YA KWARESMA

 

MWANZO:

 KUMBUKA REHEMA ZAKO(R.Kimbwi)

Kumbuka rehema zako ee Bwana kumbuka x2

 1. Kumbuka rehema zako na fadhili zako, maana zimekuwako tokea zamani.
 2. Usikumbuke makosa ya ujana wangu, wala maasi yangu ee Bwana usikumbuke.

 

BWANA UTUHURUMIE

BWANA UTUHURUMIE: (Pd. Gregory Kayetta)

((I,II) Bwana utuhurumie) - (III,IV) Bwana utuhurumie. X4

((I,II) Kristu utuhurumie) - (III,IV) Kristu utuhurumie. X2

Kristu, utuhurumie, utuhurumie Kristu.

((I,II) Bwana utuhurumie) - (III,IV) Bwana utuhurumie. X4

 

KUPELEKA NENO

NENO LITASIMAMA II

Neno litasimama, Neno litasimama, Mambo yote yatapita lakini Neno litasimama x2.

 1. Ya kale yatapita, ya dunia yatapita, mambo yote yatapita lakini neno litasimama. (Neno)
 2. Ujana utapita, usichana utapita, mambo yote yatapita lakini neno litasimama. (Neno)
 3. Ufahari utapita, na uzuri utapita, mambo yote yatapita lakini neno litasimama. (Neno)
 4. Furaha zitapita, huzuni zitapita, mambo yote yatapita lakini neno litasimama. (Neno)

 

MASOMO

Mwaka A:  

FADHILI ZA BWANA ZINA WAMCHAO

Fadhili za Bwana zina wamchao, tangu milele hata milele x2

 1. Kwa kuwa neno la Bwana lina adili/ Na kazi yake yote huitenda kwa uaminifu.
 2. Huzipenda haki na hukumu/ Nchi imejaa fadhili za Bwana.
 3. Tazama jicho la Bwana li kwao wamchao/ Wazingojeao fadhili zake.
 4. Yeye huwaponya nafsi zao na mauti/ Na kuwahuisha wakati wa njaa.

 

Mwaka B ZABURI (MISALE YA WAUMINI uk. 116)    

Nitaenenda mbele za Bwana/ Katika nchi ya walio hai.

 

Mwaka C      

BWANA NI NURU YANGU (Pd. Richard Kimbwi)

Bwana ni nuru ya uzima wa-ngu ((iii, iv) na ni ngome) Bwana ni ngome ya uzima wangu x2

 1. Umesikia, sauti yangu, unifadhili, na unijibu.
 2. Mo-yo wangu, wakuambia, u-so wako, nitautafuta.
 3. Usinifiche, u-so wako, uniokoe, mtumishi wako.
 4. U-mekuwa, msaada wa-ngu, usinitupe, ee Mungu wangu.

 

SHANGILIO

MWAKA A, B & C

SAUTI YA BABA

Sauti ya Baba ilitoka katika wingu jeupe, Huyu ni Mwanangu mpendwa, ninayependezwa naye, msikieni yeye x2

Wanafunzi waliposikia maneno hayo, walianguka kifulifuli, wakaogopa sana.

 

 MATOLEO

TOA NDUGU TOA NDUGU

Toa ndugu toa ndugu x2 ulicho nacho wewe, Bwana anakuona mpaka moyoni mwako.

 1. Sasa ndio wakati wa kutoa sadaka, kila mtu aanze kujifikiria.
 2. Wiki nzima Bwana Mungu alikulinda vema, sasa nawe ndugu yangu ujifikirie.
 3. Kumbuka jinsi Yesu alivyojitolea pale msalabani kwa ajili yetu.
 4. Tolea moyo wako, pia matendo yako, naye Bwana Mungu akubarikie.
 5. Baraka zake Mungu, za Baba na za mwana, za Roho Mtakatifu zikae nanyi nyote.

 

MTAKATIFU: (Pd. Gregory Kayetta)

((I,II) Mtakatifu Mtakatifu) - (III,IV) Mtakatifu Mtakatifu

((I,II) Bwana Mungu wamajeshi) - (III,IV) Bwana Mungu wamajeshi

((I,II) Mbingu na dunia zimejaa) - (III,IV) Mbingu na dunia zimejaa

((I,II) utukufu wako mkuu) - ((III,IV) utukufu wako mkuu.

 

((I,II) Hosana juu mbinguni) - (III,IV) Hosana juu mbinguni

((I,II) Hosana juu mbinguni) - (III,IV) Hosana juu.

Hosana, juu mbinguni, Hosana juu mbinguni.

 

((I,II) Mbarikiwa mwenye kuja) - (III,IV) Mbarikiwa mwenye kuja

((I,II) Ajaye ulimwenguni) - (III,IV) Ajaye ulimwenguni

((I,II) Kwa jina lake Bwana Mungu) - (III,IV) Kwa jina lake Bwana Mungu

((I,II) Kwa jina la Bwana Mungu) - (III,IV) Kwa jina la Bwana Mungu

 

 KUTAKIANA AMANI.

Mbinguni – kuna makao mazuri sana x2

1.Wakristo wote – tutakiane amani

Mapandre wote – tuta…

Masista wote – tuta

Wazee wote – tuta

 

 1. Wazee wote –tutakiane amani

Wamama wote – tuta

Wakaka wote – tuta

Wadada wote – tuta

 

3.Wazazi wote – tutakiane amani

Watoto wote – tuta

Vijana wote – tuta

Na ndugu wote – tuta…

 

MWANAKONDOO

 

MWANAKONDOO

3(Pd. Gregory Kayetta)

((I,II) Mwanakondoo wa Mungu) - (III,IV) Mwanakondoo wa Mungu

((I,II) Unayeondoa dhambi) - (III,IV) Unayeondoa dhambi

((I,II) dhambi zote za dunia) - (III,IV) dhambi zote za dunia

((I,II) utuhurumie Bwana) - (III,IV) utuhurumie Bwana x2

 

            ((I,II) Utujalie Amani) - (III,IV) Utujalie Amani

            ((I,II) Mwanakondoo wa Mungu) - (III,IV) Mwanakondoo

            Amani, utujalie, Utujalie Amani.

 

KOMUNYO

SAUTI YA BABA

Sauti ya Baba ilitoka katika wingu jeupe, Huyu ni Mwanangu mpendwa, ninayependezwa naye, msikieni yeye x2

 1. Wanafunzi waliposikia maneno hayo, walianguka kifulifuli, wakaogopa sana.
 2. Yesu akaja akawagusa akasema, Inukeni, wala msiogope.
 3. Wakainua macho yao wasione mtu, ila Yesu, Yesu peke yake.

 

KUSHUKURU

Twakushukuru u mwema sana

 

Twakushukuru u mwema sana Yesu asante x2

 1. Kwa kutulisha sisi -  Yesu asante,

Kwa kutunywesha sisi –

Kwa kujiunga nasi –

Kwa kutuunganisha –

 

 1. Kwa mwili wako bora –

Kwa damu yako bora –

Kwa kuja ndani yetu –

Kwa kukaa na sisi –

 

 1. Kwa mafundisho yako –

Kwa mfano wako bora –

Kwa m-salaba  wako –

Kwa ufufuko wako –

 

MWISHO

MAMA PALE MSALABANI

Mama pa-le msalabani, macho ya toka machozi

Akimwona mwanaye, kweli ni huzuni kubwa.

 1. Mwone vile akilia uchungu kama upanga, ukampenya moyowe.
 2. Mwenye moyo mgumu nani asimuhurumie basi, mama mlilia mwanawe.

 

PASIPO MAKOSA

 1. Pasipo makosa mkombozi wetu, katika baraza ya wakosefu, na wote walia asulubiwe, //aachwe Baraba na Yesu afe//x2
 2. Ee Yesu, washika msalaba wako, na unakubali kufa juu yake. Ee Yesu useme sababu gani // ya nini mateso makali hayo//x2
 3. Ni pendo la Baba wa uwinguni, ni huruma yake kwa wakosefu. We mkristu, kumbuka mateso yangu, // uache makosa, uache dhambi//x2

 

KWELI NI HUZUNI.

 1. Kweli ni huzuni, kwa kifo chake Bwana Yesu, kilivyokuwa cha maumivu, akasema moyoni, namaliza kazi kwa huzuni.

Akalia kwa huzuni, mpaka mwisho alikufa, pale juu msalabani, akakata Roho kwa huzuni x2

 1. Kweli ni ajabu, kwa kifo chake Bwana Yesu, giza likafunika nchi, tetemeko la nchi, likawa mashaka kwa watu wote.
 1. Yesu alisema, nanyi mta-teswa hivi, nami nitakuwa kati yetu, hata muwe jikoni, nitawaopoa maovuni.
Pin It