Like our Page

Yaliyopo

 

Retreat at Pfarre Gartenstadt

Dear St. Bakhita Community members,

We are all invited to a retreat @ Galvanigasse 1-3, 1210 Wien.

On 16 & 17th March 2018.

Friday: 18:00 - 20:00

Saturday: 9:00 - 20:00hrs

Retreat Master: Fr Nicholas Chileshe from Zambia.Talks will be in English and translated into Germany.All are welcome

**********

For More Details: www-gartenstadt.at

 

NYIMBO KIPINDI CHA KWARESMA

JUMAPILI YA KWANZA YA KWARESMA

 

MWANZO:

 

 ATANIITA (Pd.Gregory Kayetta)

Ataniita nami nitamwitikia, nitamwokoa na kumtukuza x2

 1. Kwa siku nyingi nitamshibisha/ nitamwokoa na kumtukuza.
 2. Ee Bwana utupe rehema zako/ ili tuyajue matendo mema ya mwanao

 

BWANA UTUHURUMIE

 

BWANA UTUHURUMIE: (Pd. Gregory Kayetta)

((I,II) Bwana utuhurumie) - (III,IV) Bwana utuhurumie. X4

((I,II) Kristu utuhurumie) - (III,IV) Kristu utuhurumie. X2

Kristu, utuhurumie, utuhurumie Kristu.

((I,II) Bwana utuhurumie) - (III,IV) Bwana utuhurumie. X4

 muziki

KUPELEKA NENO

 

NENO LITASIMAMA II

Neno litasimama, Neno litasimama, Mambo yote yatapita lakini Neno litasimama x2.

 1. Ya kale yatapita, ya dunia yatapita, mambo yote yatapita lakini neno litasimama. (Neno)
 2. Ujana utapita, usichana utapita, mambo yote yatapita lakini neno litasimama. (Neno)
 3. Ufahari utapita, na uzuri utapita, mambo yote yatapita lakini neno litasimama. (Neno)
 4. Furaha zitapita, huzuni zitapita, mambo yote yatapita lakini neno litasimama. (Neno)

 

MASOMO

Mwaka A:  ZABURI (MISALE YA WAUMINI uk. 102)

            Kiitikio: Uturehemu ee Bwana/ Kwa kuwa tumetenda dhambi.

Mwaka B       

KUMBUKA REHEMA ZAKO(R.Kimbwi)

Kumbuka rehema zako ee Bwana kumbuka x2

 1. Kumbuka rehema zako na fadhili zako, maana zimekuwako tokea zamani.
 2. Usikumbuke makosa ya ujana wangu, wala maasi yangu ee Bwana usikumbuke.

 muziki

note

Mwaka C ZABURI (MISALE YA WAUMINI uk. 108)   

Kiitikio: Ee Bwana uwe pamoja name/ katika taabu zangu.

 

SHANGILIO

MWAKA A, B & C

MTU HATAISHI KWA MKATE.

((I) Mtu hataishi kwa mkate) mtu hataishi kwa mkate, kwa mkate peke yake  ((ii) i-la)

//ila kwa kila neno litokalo kinywani mwa Mungu// x2

Nawe uzishike amri za Bwana, upate kwenda katika njia zake Bwana.

muziki 

note

 MATOLEO

 

ZAENI MATUNDA MEMA

 1. Zaeni matunda me---ma, zaeni matunda ya---le, zaeni yenye bara---ka, zaeni ya heri:

Bwana akiyapoke---ya, yatabarikiwa vye---ma zaeni matunda me---ma, zaeni ya heri x2

 1. Sarisha mwenendo wa---ko, safisha matendo ya---ko; safisha na Bwana Ye---su, safisha yo---te
 2. Fanyeni kazhi kidu---gu, fanyeni kazi kwa bi---dii, fanyeni na Bwana Ye---su, fanyeni yo---te.
 3. Tolea matunda ya---ko, pamoja na moyo wa---ko; naye Bwana Mungu wa---ko, atakubarikia.
 4. Baraka za Mungu Ba---ba, Baraka za Mungu Mwa---na, na za Roho Mtakati---fu, ziwe nanyi nyote.

 muziki

MTAKATIFU: (Pd. Gregory Kayetta)

((I,II) Mtakatifu Mtakatifu) - (III,IV) Mtakatifu Mtakatifu

((I,II) Bwana Mungu wamajeshi) - (III,IV) Bwana Mungu wamajeshi

((I,II) Mbingu na dunia zimejaa) - (III,IV) Mbingu na dunia zimejaa

((I,II) utukufu wako mkuu) - ((III,IV) utukufu wako mkuu.

 

((I,II) Hosana juu mbinguni) - (III,IV) Hosana juu mbinguni

((I,II) Hosana juu mbinguni) - (III,IV) Hosana juu.

Hosana, juu mbinguni, Hosana juu mbinguni.

 

((I,II) Mbarikiwa mwenye kuja) - (III,IV) Mbarikiwa mwenye kuja

((I,II) Ajaye ulimwenguni) - (III,IV) Ajaye ulimwenguni

((I,II) Kwa jina lake Bwana Mungu) - (III,IV) Kwa jina lake Bwana Mungu

((I,II) Kwa jina la Bwana Mungu) - (III,IV) Kwa jina la Bwana Mungu

 

 KUTAKIANA AMANI.

Mbinguni – kuna makao mazuri sana x2

1.Wakristo wote – tutakiane amani

Mapandre wote – tuta…

Masista wote – tuta

Wazee wote – tuta

 

 1. Wazee wote –tutakiane amani

Wamama wote – tuta

Wakaka wote – tuta

Wadada wote – tuta

3.Wazazi wote – tutakiane amani

Watoto wote – tuta

Vijana wote – tuta

Na ndugu wote – tuta…

 

MWANAKONDOO

MWANAKONDOO

3(Pd. Gregory Kayetta)

((I,II) Mwanakondoo wa Mungu) - (III,IV) Mwanakondoo wa Mungu

((I,II) Unayeondoa dhambi) - (III,IV) Unayeondoa dhambi

((I,II) dhambi zote za dunia) - (III,IV) dhambi zote za dunia

((I,II) utuhurumie Bwana) - (III,IV) utuhurumie Bwana x2

 

            ((I,II) Utujalie Amani) - (III,IV) Utujalie Amani

            ((I,II) Mwanakondoo wa Mungu) - (III,IV) Mwanakondoo

            Amani, utujalie, Utujalie Amani.

 

KOMUNYO

MTU HATAISHI KWA MKATE.

((I) Mtu hataishi kwa mkate) mtu hataishi kwa mkate, kwa mkate peke yake  ((ii) i-la)

//ila kwa kila neno litokalo kinywani mwa Mungu// x2

 1. Nawe uzishike amri za Bwana, upate kwenda katika njia zake Bwana.
 2. Bwana ni mkate ule wa uzima, tumpokee tupate neema za mbinguni.
 3. Bwana ni uzima wa mwili na Roho, anashibisha Roho na mema ya mbinguni.
 4. Bwana atupenda sisi watu wake, tujitakase kweli kwa toba na mfungo.

muziki 

note

KWELI BAHATI

Kweli bahati ilioje (ii,iii, kweli) kujongea meza ya Bwana x2

 1. Ninapokula mwili wa Bwana (ii, Yesu), Ninapokunywa damu ya Bwana (ii, Yesu), Ninapata uzima mpya.
 2. Meza ya Bwana sasa tayari (ii, twende), Anatuita tukampokee (ii, Bwana), tutapata uzima mpya.
 3. Mwili wa Bwana chakula bora (ii, kweli), Damu ya Yesu kinywaji bora (ii, sana), chakula chetu wasafiri.

 

KUSHUKURU

 

ASANTE BWANA YESU

(I, Asante Bwana Yesu) //kwa mema yako (iv, yote) kwa mema yako, uliyo tujaliya (iv, asante) kwa mema yako (iv, yote) kwa mema yako, uliyo tujaliya.

 1. Umetulisha, umetunywesha, twa-shukuru.
 2. Mema ya mbingu, tumeyapata, twa-shukuru.
 3. Mwana wa Mungu, u kati yetu, twa-shukuru.
 4. Kwa vitu vyote, ulivyotupa, twa-shukuru.

 

MWISHO

MAMA PALE MSALABANI

Mama pa-le msalabani, macho ya toka machozi

Akimwona mwanaye, kweli ni huzuni kubwa.

 1. Mwone vile akilia uchungu kama upanga, ukampenya moyowe.
 2. Mwenye moyo mgumu nani asimuhurumie basi, mama mlilia mwanawe.

 muziki

PASIPO MAKOSA

 1. Pasipo makosa mkombozi wetu, katika baraza ya wakosefu, na wote walia asulubiwe, //aachwe Baraba na Yesu afe//x2
 2. Ee Yesu, washika msalaba wako, na unakubali kufa juu yake. Ee Yesu useme sababu gani // ya nini mateso makali hayo//x2
 3. Ni pendo la Baba wa uwinguni, ni huruma yake kwa wakosefu. We mkristu, kumbuka mateso yangu, // uache makosa, uache dhambi//x2

 

Pin It