Like our Page

Yaliyopo

 

Retreat at Pfarre Gartenstadt

Dear St. Bakhita Community members,

We are all invited to a retreat @ Galvanigasse 1-3, 1210 Wien.

On 16 & 17th March 2018.

Friday: 18:00 - 20:00

Saturday: 9:00 - 20:00hrs

Retreat Master: Fr Nicholas Chileshe from Zambia.Talks will be in English and translated into Germany.All are welcome

**********

For More Details: www-gartenstadt.at

 

MAAJILIO

TAZAMA ANAKUJA BWANA

Tazama anakuja Bwa-na, mtawa-la, mwenye ufalme mabegani mwake (iv: na uweza) na E-------nzi x2

1. Ondoka ee Yerusalemu uangaze, kwa kuwa nuru yako imekuja, na utukufu wa Mungu utakung’aria.

 

NJOO KWETU MASIHA.

Njoo kwetu Masiha (njoo) njoo Bwana utuokoe x2

1. Utuhurumie sisi wa dhambi, tunakulilia tusikilize

2. Nungu za shetani zimetubana, njia ya uwingu haipitiki.

3. Utufungulie mlango wa mbingu, na kuyatakasa maovu yote.

4. Nazo dhambi zetu zimetusonga, kamba za mauti zatuzunguka.

 

XMASS

KAZALIWA MTOTO

Kazaliwa Mtoto, mkombozi wetu x2 Tumshangilia mtoto kazaliwa x2

1. Pa – ngoni Betrehemu – Tumshangilie mtoto kazaliwa,

Mjini mwa Daudi - Tumshangilie mtoto kazaliwa

2. Kaja kutukomboa–

Yeye mkombozi wetu–

3. Tuimbe na kucheza –

Ma – siha kazaliwa –

 

NJONI WAPENZI TUFANYE SHANGWE.(12-8)

a. Njoni wapenzi tufanye shangwe – Mwokozi Bwana amezaliwa / Viumbe vyote tufanye shangwe - Mwokozi Bwana amezaliwa

Natufanye shangwe, twimbe aleluya, Mwokozi Bwana amezaliwa.

b. Malaika alitutangazia – Mwokozi Bwana amazaliwa / Furaha yetu ni kubwa sana–

c. Tuende pamoja na wachungaji – / Tumwone mtoto Yesu Pangoni –

d. Yeye ni kweli Mwana wa Mungu –/ Mapendo yake hayana mwisho –

e. Hii ni siku ya furaha kuu – / Mungu mwenyewe atushukia–

f. Tufanye shangwe kwa nyimbo nzuri – / Tumsifu Bwana na kumshukuru–

g. Sisi kwa sisi na tupendan

 

BWANA YESU KAZALIWA (12-9)

Bwana Yesu kazaliwa tumwimbie kwa furaha aleluya Aleluya aleluya aleluya aleluya aleluya.

1. Kwa ajili yetu sisi, amezaliwa kitoto aleluya.

2. Amezaliwa kitoto, nasi tumepewa Mwana aleluya.

3. Utawala na uwezo, vipo mabegani mwake aleluya.

4. Jina lake ndilo Baba, wa umilele tena mfalme aleluya.

5. Enzi yake ya kifalme, haitakuwa na mwisho aleluya.

6. Anakalia kitiye, chake Daudi babaye aleluya.

7. Furaha binti Sioni, umpokee Bwana wako aleluya

 

JONGEENI WAKRISTU (12-5)

a. Jongeeni wakristu, furahini sana, jongeeni jongeeni Betlehemu. Mfalme wa mbingu kaja duniani – Jongeeni kumwabudu, Jongeeni kumwabudu, Jongeeni kumwabudu Yesu Kristu.

b. Waona wachunga malaika wa Mungu, wasikia sauti za uwingu, Na sisi twende Btlehem pangoni. Jongeni …

c. Mapendo makubwa Yesu atupenda, ametukomboa kwa mapendo. Tumpende pia kweli kwa vitendo. Jongeni …

 

MBALI KULE NASIKIA (12-3) Lk. 2,14)

a. Mbali kule nasikia malaika wa mbinguni, Wakimba wengi pia wimbo huu juu angani, Glo - - - ria in excelsis De – o x2

b. Wachunga tuambieni sababu ya nyimbo hizo; mwenye kwimbiwa ni nani, juu ya nani sifa hizo?

c. Je, hamjui jambo kuu la kuzaliwa Mwokozi? Habari ya wimbo huu ndiyo kumshukuru Mwenyezi.

d. Kweli, nasi twende hima, tufike kule aliko, tuone mtoto na mama, tuwasalimie huko.

 

NENO ALIFANYIKA MWILI

Neno alifanyika mwi – li, nasi tukauona utukufu wake x2

a. Utukufu wake yeye, aliye mwana wa Baba.

b. Amejaa neema na kweli, aliye mwana wa Baba.

c. Yeye ndiye mwana kweli, ajaye ulimwenguni.

d. Huo ndio Mwanga kwetu, ajaye ulimwenguni.

e. Awaangazia wote, waone iliyo kweli.

 

HERI MTOTO YESU

He – ri, He – ri Mtoto Yesu x2 Heri maziwa, uliyo nyonya, Heri na tumbo lililokuza… x2

a. Amezaliwa leo kweli Mtoto Yesu, Mwana wa Mungu Yesu kaja tukomboa, Tumwimbie Mtoto Yesu kazaliwa.

b. Malaika wa Mbingu wamwimbia Mtoto, amezaliwa leo Pangoni Betrehemu, tumwimbie Mtoto Yesu kazaliwa.

c. Na sisi twende hima tukamwone Mtoto, Mwana wa Mungu Yesu aliyezaliwa, tumwimbie kwa furaha kazaliwa.

d. Nyimbo nzuri na ngoma, tuimbe tucheze, tumshangilie Mtoto aliyezaliwa, tumwimbie kwa furaha kazaliwa.

 

YESU MWANA WA MUNGU

Yesu Mwana wa Mungu, Yesu Mwana wa Mungu leo amezaliwa Piga vigelegele, piga vigelegele, leo amezaliwa

a. Agano latimia, Mwokozi kazaliwa Yesu, Mwana wa Mungu, kweli amezaliwa

b. Pangoni Betlehemu, amezaliwa Yesu Yeye ni ndugu yetu, pia Mkombozi wetu

c. Japo yeye ni mfalme, kajifanya maskini Muumba wa vitu vyote, twende tufike kwake

d. Maria mamaye, Yosef ni mlishi wake Nasi sote nduguze, twende, tufike kwake

e. Mbingu na zifurahi, nchi ishangilie Bahari na ivume, na vyote ndani yake.

 

UBATIZO WA BWANA

SAUTI YA BABA

Sauti ya Baba ilitoka katika wingu jeupe, Huyu ni mwanangu mpendwa, ninayependezwa naye, msikieni yeye x2.

1. Bwana alipokwi-sha kubatizwa, mbingu zikamfunikia, Roho wa Bwana akashuka, kwa mfano wa hua.

2. Roho akashuka kwa mfano wa hua, na kukaa juu yake, juu ya Bwana Yesu.

Pin It