TWAKUSHUKURU (KIMBWI)
Twakushukuru ee Mungu Baba muumba wa vyote, umetulinda tuko salama tunakushukuru x2.
1. Umetulisha chakula Bwana, umetulinda tuko salama tunakushukuru.
2. Kwa wiki nzima umetulisha, umetulinda tuko sama tunakushukuru.
3. Baraka zako utujalie, umetulinda tuko salama tunakushukuru.
Twakushukuru u mwema sana
Twakushukuru u mwema sana Yesu asante x2
1. Kwa kutulisha sisi - Yesu asante, Kwa kutunywesha sisi – Kwa kujiunga nasi – Kwa kutuunganisha –
2. Kwa mwili wako bora – Kwa damu yako bora – Kwa kuja ndani yetu – Kwa kukaa na sisi–
3. Kwa mafundisho yako – Kwa mfano wako bora – Kwa m-salaba wako – Kwa ufufuko wako –
ASANTE BWANA YESU
(I, Asante Bwana Yesu) //kwa mema yako (iv, yote) kwa mema yako, uliyo tujaliya (iv, asante) kwa mema yako (iv, yote) kwa mema yako, uliyo tujaliya.
1. Umetulisha, umetunywesha, twa-shukuru.
2. Mema ya mbingu, tumeyapata, twa-shukuru.
3. Mwana wa Mungu, u kati yetu, twa-shukuru.
4. Kwa vitu vyote, ulivyotupa, twa-shukuru.
TWAKUSHUKURU EE BWANA.
Twakushukuru ee Bwana muumba wa vyote, asante kwa mema yote uliyotujalia x2
1. Umenilinda vyema, katika maisha, umenijalia na afya njema mwilini / umenilisha mwili na damuyo Bwana, umenijalia na afya njema mwilini.
2. Umenipa maisha, nikutumikie, ili nitangaze wema na upendo wako / umenipa uwezo, nikutumikie, nitangaze duniani kote wema wako.
3. Furaha yangu Bwana, tumaini langu, kutangaza neno lako hapa duniani / akili yangu Bwana, na uwezo wangu, vyote mali yako Bwana nakutumikia.