Like our Page

Yaliyopo

Retreat at Pfarre Gartenstadt

Dear St. Bakhita Community members,

We are all invited to a retreat @ Galvanigasse 1-3, 1210 Wien.

On 16 & 17th March 2018.

Friday: 18:00 - 20:00

Saturday: 9:00 - 20:00hrs

Retreat Master: Fr Nicholas Chileshe from Zambia.Talks will be in English and translated into Germany.All are welcome

**********

For More Details: www-gartenstadt.at

KWELI BAHATI

Kweli bahati ilioje (ii,iii, kweli) kujongea meza ya Bwana x2

1. Ninapokula mwili wa Bwana (ii, Yesu), Ninapokunywa damu ya Bwana (ii, Yesu), Ninapata uzima mpya.

2. Meza ya Bwana sasa tayari (ii, twende), Anatuita tukampokee (ii, Bwana), tutapata uzima mpya.

3. Mwili wa Bwana chakula bora (ii, kweli), Damu ya Yesu kinywaji bora (ii, sana), chakula chetu wasafiri.

KARIBU MOYONI MWANGU LEO

Karibu moyoni mwangu leo, Yesu wangu mpenzi Ukaye na mimi siku zote, zamaisha yangu. x2

1. Nikitazama pande zote, pande za dunia, nawaona wote, wamejaa, furaha moyoni. Nami pia ninatamani, kuwa nawe Bwana, iliniungane, na wataka-tifu wa Mbinguni.

2. Bwana ndiwe furaha yangu, na uzima wangu, uungane nami, siku zote za maisha yangu. Bila wewe sina amani, hapa duniani, kaa nami Bwana, siku zote, za maisha yangu.

3. Duniani sina amani, bila wewe Bwana, karibu moyoni, mwangu leo, ewe Bwana wangu. Safarini niwe salama, kuja kwako Bwana, ili niungane, na wataka-tifu wa Mbinguni.

KARIBU MOYONI MWANGU LEO

Karibu moyoni mwangu leo, Yesu wangu mpenzi Ukaye na mimi siku zote, za maisha yangu. x2

1. Nikitazama pande zote, pande za dunia, nawaona wote, wamejaa, furaha moyoni. Nami pia ninatamani, kuwa nawe Bwana, iliniungane, na wataka-tifu wa Mbinguni.

2. Bwana ndiwe furaha yangu, na uzima wangu, uungane nami, siku zote za maisha yangu. Bila wewe sina amani, hapa duniani, kaa nami Bwana, siku zote, za maisha yangu.

3. Duniani sina amani, bila wewe Bwana, karibu moyoni, mwangu leo, ewe Bwana wangu. Safarini niwe salama, kuja kwako Bwana, ili niungane, na wataka-tifu wa Mbinguni.

POKEA MOYO WANGU

1. Onjeni mwone kwamba Bwana yu mwema, na heri mtu Yule, anayemtumaini Yesu Kristo.

Pokea moyo wangu ee Mungu wangu, niweze kukupenda kwa pendo lako // unipe moyo wako, ewe Yesu Mkombozi wangu shinda kwangu nami daima kwako //x2

2. Katika nguvu za giza katutoa, na kutukaribisha , katika ufalme wa pendo lake.

3. Habari njema alituhubiria, na kutufungulia, akatangaza mwaka wa neema.

4. Mchungaji wangu mkuu ndiye Bwana Yesu, sikosi kitu kwamwe, huniongoza kwenye njia nyofu.

5. Baraka na heshima na utukufu, na uweza kwa yeye, Mwanakondoo wa Mungu milele.

TUMWANGUKIE YESU NA MOYO WAKE MKUU

Tumwangukie Yesu na Moyo wake mkuu x2// Tumpende tumshukuru milele tumsifu x2

1. (I,ii) Kuliko nyoyo zote ni mmoja moyo mkuu, mapendo yake kwetu hayana kifani // Tumpende tumshukuru milele tumsifu x2

2. Ee Moyo wa huruma wa Yesu mkombozi, umetupa wokovu kwa kufa mtini. // Tumpende tumshukuru milele tumsifu x2

3. Kisima cha furaha na cha fara-ja kuu, tukitamani Roho tuje ku-teka tuu. // Tumpende tumshukuru milele tumsifu x2

Pin It