ROHO NDIYO ITIAYO UZIMA (Zaburi)
((i) Roho ndiyo itiayo uzima, mwi-li haufai kitu) Maneno hayo niliyo waambia ni roho, tena ni uzi-ma.
1. Sheria ya Bwana ni kamilifu, huiburudisha nafsi/ ushuhuda wa Bwana ni amini, humtia mjinga hekima.
2. Maagizo ya Bwana ni adili, huufurahisha moyo/ Amri ya Bwana ni safi huyatia macho nuru.
3. Kicho cha Bwana ni kitakatifu, kinadumu milele/ Hukumu za Bwana ni kweli zina haki kabisa.
4. Maneno ya kinywa change na mawazo ya moyo wangu/ yapate kibali mbele yako ee Bwana Mwamba wangu na Mwokozi wangu.
KUMBUKA REHEMA ZAKO
Kumbuka rehema zako ee Bwana kumbuka x2
a. Kumbuka rehema zako na fadhili zako, maana zimekuwako tokea zamani.
b. Usikumbuke makosa ya ujana wangu, wala maasi yangu ee Bwana usikumbuke.
c. Adui zetu bwana wasitushinde, Mungu wa Israel Bwana utuokoe.
MTU AKINITUMIKIA
Mtu akinitumikia Ba-ba yangu aliye juu Mbinguni atamuheshimu, asema Bwa-na x2
1. Mkilaumiwa wa ajili ya jina langu ni heri yenu/ kwa maana utukufu wa Mungu unawakalia.
2. Ee Bwana unifundishe njia ya amri zako/ nami nitaishika hata mwisho.
3. Unifahamishe nami nitaishika sheri yako/ naam, nitaitii kwa moyo wangu wote,
BWANA AMETAMALAKI
Bwana ameta-mala-ki, ametamala-ki (II: malaki), nchi na ishangili-e, i-shangilie x2.
1. Mbingu na zifurahi, na zitangaze, haki yake mwenyezi, ukuu wake.
2. Bwana ndiye mkuu, uliye juuu, juu sana ee Bwana, kuliko yote.
3. Bwana umetukuka, juu ya vyote, umetukuka Bwana, mtakatifu.
NITAKUIMBIA (Zaburi)
Mbele ya miungu nitakuimbia (ii,iii zaburi) x2.
1. Bwana huishika kweli milele, Huwafanyia hukumu walioone-wa/ Huwapa wenye njaa chakula, Bwana hufungua waliofungwa.
2. Bwana huwafumbua macho waliopofuka, Huwainua walioina-ma/ Bwana huwapenda wenye haki, Huwahifadhi wageni.
3. Bwana huwategemeza yatima na mjane, Bali njia ya wasio haki huipotosha/ Bwana atamiliki milele, Mungu wako Ee Sayuni kizazi hata kizazi.
FADHILI ZA BWANA ZINA WAMCHAO
Fadhili za Bwana zina wamchao, tangu milele hata milele x2
1. Heri aliyesamehewa dhambi, na kusitiriwa makosa yake/ Heri Bwana asiyemhesabia upotovu, ambaye rohoni mwake hamna hila.
2. Nalikujulisha dhambi yangu, wala sikuuficha upotovu wangu/ Nalisema nitayakiri maasi yangu kwa Bwana, nawe ukanisamehe upotovu wa dhambi yangu.
3. Mfurahieni Bwana, shangilieni enyi wenye haki/ pigeni vigelegele vya furaha, ninyi nyote mlio wanyofu wa moyo.
FADHILI ZA BWANA NITAZIIMBA.
Fadhili za Bwana nitaziimba milele. Fadhili za Bwana nitaziimba mi-lele x2
1. Maana nimesema fadhili zitajengwa fadhili zitajengwa zitajengwa milele.
2. Katika m-bingu utauthibiti-sha utauthibitisha uaminifu wako.
3. Nimefanya aga-no na mteule wa-ngu nimemwapia Dau-di mtumishi wangu.
4. Wazao wako ni-tawafanya imara mile-le nitakijenga kiti cha-ko cha enzi mile-le.
MWIMBIENI BWANA WIMBO MPYA.
Mwi – mbieni Bwana wimbo mpya, Mwi – mbieni Bwana nchi yote //Mwimbieni Bwana libarikini jina lake//x2
1. Tangazeni wokovu wake siku kwa si – ku/ Wahubirini mataifa habari za utuku-fu wa-ke.
2. Mbingu na zifurahi nchi na i-shangili – e/ bahari na ivume na vyote vi – ijaza – vyo.
3. Mashamba na yashangilie na vyote vilivyo – mo/ ndipo miti yote ya mwituni iimbe kwa fura – ha.
4. Mbele za Bwana kwa maana anaku – ja/ anakuja ili aihukumu n – chi.
5. Atauhukumu ulimwengu kwa ha – ki/ na mataifa kwa uami – ni-fu wa – ke.
ENYI MATAIFA MTUKUZENI MUNGU.
Enyi mataifa, mtukuzeni Mungu x2 Itangazeni sauti ya sifa yake, enyi mataifa mtukuzeni Mungu.
1. Nalimwita Bwana kwa kinywa changu/ Naye akasikia sauti ya dua zangu.
2. Asifiwe Mungu asiyekataa/ maombi ya dua zangu.
3. Hakuninyima huruma yake/ fadhili zake hakuniondolea.