Like our Page

Yaliyopo

 

Retreat at Pfarre Gartenstadt

Dear St. Bakhita Community members,

We are all invited to a retreat @ Galvanigasse 1-3, 1210 Wien.

On 16 & 17th March 2018.

Friday: 18:00 - 20:00

Saturday: 9:00 - 20:00hrs

Retreat Master: Fr Nicholas Chileshe from Zambia.Talks will be in English and translated into Germany.All are welcome

**********

For More Details: www-gartenstadt.at

 

BWANA UTUHURUMIE

(i: Bwana bwana utuhurumie ee Bwana) //Bwa - na bwana bwa – na, Bwa – na utuhurumie (iv: ee Bwana)//x2

(i: Kristu Kristu utuhurumie ee Bwana) //Kri - stu Kristu Kri – stu, Kri – stu utuhurumie

(iv: ee Kristu)//x2

 

BWANA UTUHURUMIE KWANI TUMEKUKOSEA (Misa ya Mt. Charles)

Bwana utuhuru- mie, kwani tumekukosea Bwa – na, tuhurumie Bwa-na x2

(iv. Kristu utuhurumie) Kwani tumekukosea Kri – stu, utuhurumie Kris – stu x2

Bwana utuhuru- mie, kwani tumekukosea Bwa – na, tuhurumie Bwa-na x2

note

 

UTUKUFU KWA MUNGU MBINGUNI

(I, Utukufu kwa Mungu mbinguni) Utukufu kwako Mungu mbinguni, na amani pote duniani kwao watu wa mapenzi me-ma.

1. Tunakuheshimu, tunakusifu/ tunakuabudu, twakutuza, ee Bwana–

2. Tunakushukuru, mfalme wa mbingu/ Mwana wa pekee, Mwana wa Baba, ee Bwana–

3. Unayeondoa makosa yetu/ utuhurumie, ‘tusikilize, ee Bwana–

4. Kuume kwa Baba unapoketi/ Mtakatifu Mkuu ‘tuhurumie, ee Bwana–

5. Roho Mtakatifu pamoja nawe/ ndani yake Baba unatukuzwa, ee Bwana –

 

UTUKUFU(Misa ya Mt. Charles) (Fr. Richard Kimbwi)

Utukufu (iv,utukufu) kwa Mungu juu (ii,iv, mbinguni) Na amani (iii,iv,amani) duniani, kwa watu wenye mapenzi me – ma x2

1. Tunakusifu tunakuheshimu, twakuabudu tunakutukuza. Twakushukufu kwa a-jili, ya utukufu wako Mkuu.

2. Ee Bwana Mungu, Mfalme wa mbinguni, wewe ni Mungu Baba Mwenyezi. Ee Yesu Kristo mwana wake Baba, Mwanakondoo wa Mungu, mwana wa Baba.

3. Uondoaye dhambi za dunia, tuhurumie pokea ombi letu. Mwenye kuketi kuume kwa Baba, tuhurumie utuhurumie.

4. Kwa kuwa ndiwe peke Mtakatifu, pekee Bwana mkuu Yesu Kristo. Pamoja naye Roho Mtakatifu, utukufu wa Mungu Baba A-MINA.

 

UTUKUFU KWA MUNGU JUU

Utukufu kwa Mungu juu na amani duniani //kwa watu wenye mapenzi mapenzi mema x2.

1. Tunakusifu tunakuheshimu, Twakuabudu tunakutukuza/ Twakushukuru Bwana kwa ajili, ya utukufu wako Bwana Mkuu.

2. Ee Bwana Mungu Mfalme wa Mbinguni, wewe ni Mungu na Baba Mwenyezi./ Ee Bwana Yesu mwana wa pekee, Mwanakondoo ni Mwana wa Baba

3. Uondoaye dhambi za dunia, tuhurumie pokea maombi/ Mwenye kuketi kuume kwa Baba, tuhurumie utuhurumie.

4. Kwaku ndiye peke Mtakatifu, pekee Bwana Mkuu Yesu Kristo / Pamoja naye Roho Mtakatifu, utukufu wake Baba. Amina

 

NASADIKI. (Pd. Gregory Kayetta)

Ninasadiki ninasa-di-ki, ninasadiki nina-sa-di-ki, ninasadiki ninasadiki.

1. -Mungu Baba muumba wa vyote, nasadiki kwa mwanawe Yesu Kristo – Ninasadiki ninasadi-ki. -Kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, hapo Maria akamzaa Yesu – Ninasadiki ninasadi-ki.

2. -Kateswa kwa mamlaka ya Pilato, akasulibiwa kafa akazikwa – k’shuka kuzimu ninasadi-ki. -Siku ya tatu akafufuka, akapaa mbinguni kwa Mungu Baba - a’kaa kuume kwake ninasadi-ki.

3. -Tarudi tena siku ya mwisho, kuwahukumu wazima na wafu – ufalme wake hauna mwisho. -Nasadiki kwa Roho Mtakatifu, Bwana mleta uzima abudiwa – na kutukuzwa ninasadi-ki.

4. -Nasadiki kwa kanisa moja, Takatifu Katoliki la mitume – ninasadiki ninasadi-ki. -Nangojea ufufuko wa wafu, na uzima wa milele ijayo – A---mina ninasadi-ki.

 

MTAKATIFU(Misa ya Mt. Charles) (Pd. Richard Kimbwi)

Mtakatifu mtakatifu Bwana, Mtakatifu Bwana Mungu wa majeshi //Mbingu na nchi zimejaa utukufu wako x2

Hosana Hosa – na (ii,iii, Hosana) Hosana Hosa – na, Hosana Hosa - na juu Mbinguni x2

Mbarikiwa yeye mwenyeku-ja, anayeku-ja kwa jina la Bwana.

note

 

MTAKATIFU

(iv: Mtakatifu), Mtakatifu, mtakatifu, Bwana Mungu

(iv: wa majeshi) Mbingu na dunia zimejaa ‘tukufu wako.

//(iii: Hosa-na) hosana juu mbinguni (iii: hosana) hosana juu mbinguni//x2

//(iv: Mbarikiwa) anayekuja kwa jina la lake Bwana Mungu//x2

 

MWANAKONDOO

(i: Ee Mwanakondoo) uondoaye dhambi za dunia utuhurumie //x2

(iii: Ee Mwanakondoo) uondoaye dhambi za dunia utujalie amani.

 

MWANAKONDOO

(Mwanakondoo wa Mungu uondoaye) dhambi za dunia utuhurumie utuhurumie x2

(Mwanakondoo wa Mungu uondoaye) dhambi za dunia utupe amani utupe amani.

 

NENO LITASIMAMA II

Neno litasimama, Neno litasimama, Mambo yote yatapita lakini Neno litasimama x2.

1. Ya kale yatapita, ya dunia yatapita, mambo yote yatapita lakini neno litasimama.

2. Ujana utapita, usichana utapita, mambo yote yatapita lakini neno litasimama.

3. Ufahari utapita, na uzuri utapita, mambo yote yatapita lakini neno litasimama.

4. Furaha zitapita, huzuni zitapita, mambo yote yatapita lakini neno litasimama.

 

KUTAKIANA AMANI.

Mbinguni – kuna makao mazuri sana x2

1.Wakristo wote – tutakiane amani

Mapandre wote – tuta…

Masista wote – tuta…

Wazee wote – tuta…

2. Wazee wote – tutakiane amani

Wamama wote – tuta…

Wakaka wote – tuta…

Wadada wote – tuta…

3.Wazazi wote – tutakiane amani

Watoto wote – tuta…

Vijana wote – tuta…

Na ndugu wote – tuta…

Pin It